Exodus 31

Bezaleli Na Oholiabu

(Kutoka 35:30–36:1)

1Ndipo Bwana akamwambia Musa, 2 a“Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, 3 bnami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, 4ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, 5kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi. 6 cTena nimemteua Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, ili kumsaidia. Pia mafundi wote nimewapa ustadi wa kutengeneza kila kitu nilichokuamuru wewe: 7 dHema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda pamoja na kiti cha rehema juu yake, pia na vifaa vyote vya kwenye hema, 8 emeza na vifaa vyake, kinara cha taa cha dhahabu safi na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba, 9 fmadhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, sinia na kinara chake, 10 gpamoja na mavazi matakatifu yaliyofumwa ya kuhani Haruni, na mavazi kwa ajili ya wanawe wakati wanahudumu katika kazi ya ukuhani, 11 hpia mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri kwa ajili ya Mahali Patakatifu. Watavitengeneza sawasawa kama vile nilivyokuagiza wewe.”

Sabato

12Kisha Bwana akamwambia Musa, 13 i“Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni lazima mzishike Sabato zangu. Hii itakuwa ni ishara kati yangu na ninyi kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili mpate kujua kwamba Mimi Ndimi Bwana, niwafanyaye ninyi watakatifu.

14 j“ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Yeyote atakayeinajisi lazima auawe, yeyote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akafie mbali na watu wake. 15 kKwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, takatifu kwa Bwana. Yeyote afanyaye kazi yoyote siku ya Sabato ni lazima auawe. 16 lWaisraeli wataishika Sabato, kuiadhimisha kwa vizazi vijavyo kuwa Agano la milele. 17 mItakuwa ishara kati yangu na Waisraeli milele, kwa kuwa kwa muda wa siku sita Bwana aliumba mbingu na dunia, na siku ya saba akaacha kufanya kazi, akapumzika.’ ”

18 n Bwana alipomaliza kusema na Musa juu ya Mlima Sinai, Mungu akampa vile vibao viwili vya Ushuhuda, vibao vya mawe vilivyoandikwa kwa kidole cha Mungu.
Copyright information for SwhKC